DC UBUNGO: ACHENI KUJENGEA MAKABURI, NAFASI ZINAJAA

0

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, Kheri James ameshauri kuwa ni wakati sasa wa kuacha tamaduni ya kujengea makaburi hasa yale ya jumuia.

Kiongozi huyo alikuwa ni mmoja wa wananchi waliojitokeza katika usafi wa Makaburi ya Sinza A, leo Jumamosi asubuhi, shughuli ambayo iliratibiwa na Kituo cha Radio Times FM ikishirikisha wafanyakazi wa kituo hicho pamoja na wakazi wa Sinza na maeneo ya karibu.

SOMA HII:TAARIFA MPYA YA POLISI WALIOUAWA DAR;

Akizungumza katika eneo la tukio, Kheri James alisema: “Tunayo changamoto ya makaburi kujaa katika maeneo tofauti, haya maeneo ya mjini haya ambayo makaburi yanajaa, kumekuwa na desturi kila mmoja anapozika ndugu yake anajenga.


“Kuna haja sasa katika maeneo yetu ya Dar hasa wilaya yetu ya Ubungo kuanza kuondoa utamaduni wa kujengea kila kaburi tunalozika wapendwa wetu.


“Nadhani kama ni kujenga iwe inafanywa hivyo katika yale makaburi ya binafsi, mfano ya kanisa, misikiti, familia nakadhalika.


“Lakini haya ya jumuiya haya kila mmoja akisema ajenge, ndugu zangu nawaambia itashindikana na nafasi zitajaa, kuna ushuhuda hapa mmeukuta (Sinza Makaburini) viungo vya marehemu vikiwa juujuu ya ardhi, hiyo ni kwa kuwa mazingira yanaonyesha kumejaa.


“Nitoe wito pia kwa wale wachimbaji kuwa wakikuta viungo vya marehemu kama hivyo, wahifadhi salama kuliko kuacha kuona vikiwa vimezagaa hovyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top