Leo Agosti 23 2021 kumeripotiwa ajali tatu tofauti ambapo mpaka sasa watu watano wamethibishwa kufariki dunia huku wengine wakipata majeraha katika matukio hayo matatu tofauti.
![]() |
Picha kutoka ajali ya wafanyakazi was TRA. |
Mapema asubuhi hii Leo tunepokea taarifa ya majonzi juu ya Vigo vya watumishi wa TRA mkoani Songwe!
Taarifa zaidi SOMA HII..WATUMISHI WATANO TRA WAFA AJALINI
Huko mkoani Pwani tumekuletea taarifa hii kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa ajali leo asubuhi katika eneo la Kwa Mbonde, Kata ya Picha ya Ndege, Kibaha baada ya Basi la Sauli ambalo lilikuwa linatokea Dar es salaam kwenda Tunduma kuacha njia na kutoka nje ya barabara kama mita kumi kisha likagonga Scania lililobeba mchanga.
RPC Nyigesa amesema Watu wanne wamepata michubuko kutokana na ajali hiyo na kufikishwa Tumbi Hospitali ambako wametibiwa na kuruhusiwa.
“Chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Sauli kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari(Wrong Overtaking) akaacha Barabara Wataalamu wanaita kuchochora, majeruhi kwenye ajali hiyo ni wanne na wote wametibiwa na kuruhusiwa” ———Nyigesa.
Ajali ya tatu imehusisha gari la mizigo ambapo,dereva wa Lori la mizigo lililokua likitoka Dar es salaam kuelekea nchini Zambia amepata majeraha kidogo baada ya Lori alilokuwa akiliendesha kupinduka maeneo ya Kimara Dar es salaam na kusababisha foleni karibu na eneo la ajali,
akiongea na @AyoTV_ Dereva huyo amesema chanzo cha ajali ni kumkwepa bodaboda ambapo Trela ndio likayumba na kusababisha lori hilo kuanguka, Polisi wamewataka Madereva kuangalia njia mbadala wakati jitihada za kuliinua lori zinaendelea.