ISIKUPITE TAARIFA HII KUTOKA JESHI LA POLISI KATAVI

0

 


JESHI  la Polisi  mkoani Katavi, linamshikilia Mathias Sikazwe (68) kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya tembo akiwa ameyahifadhi kwenye banda la kufugia mbuzi.


Akizungumza na Waandishi wa habari leo Kamanda wa jeshi hilo, Benjamin Kuzaga, amesema tukio hilo limetokea Agosti 03,2021 katika Kijiji cha Igongwe kata ya Stalike mkoani humo.


Amesema kwa kushilikiana na kikosi cha hifadhi ya Taifa ya Katavi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema  na kufanya msako katika nyumba yake na kufanikiwa kumkamata.


"Meno hayo yana uzito wa kg 2.5 ambayo thamani yake bado haijajulikana ila tuna hesabu kwamba alimuua tembo mzima mwenye thamani ya fedha za kimarekani  dola Elfu 20. ", amesema Kuzaga.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top