KAGERA-WATU WATANO WAMEKUFA KATIKA AJALI.

0

  Watu watano wamepoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kasindaga, wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.


Ajali hiyo imeyahusisha gari la abiria lenye namba za usajili T567 DFA mali ya kampuni ya Frester lililokuwa likitoka mkoani Morogoro kuelekea Bukoba mkoani Kagera, baada ya kugongana na gari dogo aina ya Corora lenye namba za usajili T741 AXY lilikuwa likitoka wilaya ya Muleba kuelekea mkoani Geita.


Mganga Mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo Dk. Gresmus Sebuyoya amesema wamepokea miili ya watu watano, ambayo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.


Dk. Sebuyoya ametaja majina ya marehemu hao kuwa ni Majid Abubakar, Mdathiru Hashim, Julian Julius, John Method na mwingine amefahamika kwa jina moja la Fravius, wote wanaume.


Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alikuwa akiendesha kwa kasi na kusababisha kuhama katika sehemu yake na kwenda kugongana uso kwa uso na gari hilo dogo.

Tazama picha za tukio la Ajali hapa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top