Kulikuwa na hali ya kushangaza katika Hospitali ya Rufaa ya Bungoma mwili wa mwanamuziki Peter Oteng alimaarufu Storm Dwarchild ulipokataa kuingia katika jeneza kwa kutaka jeneza la bei ghari.
Oteng ambaye pia alikuwa afisa wa mawasiliano wa mbunge wa Kanduyi, Wafula Wamunyinyi, mwili wake ulikataa kutoshea kwenye jeneza hadi lingine la bei ghali liliponunuliwa.
Rafiki yake alisema huenda alikataa kuwekwa katika sanduku hilo kwa sababu pesa nyingi zilichangwa ili afanyiwe mazishi ya hadhi, Oteng alipatikana ameuawa na mwili wake kutupwa kando ya viungani vya mji wa Bungoma.
Swahiba huyo pia alidai kuwa huenda waliomuua Oteng walikuwepo katika mochari hiyo na hivyo alikasirika kuwoana.
"Kunaweza kuwa na sababu nyingi za kufanya akose kuingia katika jeneza. Pengine familia yake na jamaa kutoka Uganda walikasirika na kufanya tambiko kuhakikisha kuwa wauaji wake hawatakuwa na amani maishani," rafiki huyo alisema.
Source: TUKO