![]() |
Picha kutoka Maktaba |
Mbunge wa jimbo la Sengerema Tabasam Hamis Mwagao anaendelea na ziara yake ya kuwashukuru wananchi jimboni humo kwa kumchangua, ambapo amefika katika kata ya Buzirasoga na kukutana na changamoto ya Shule ya msingi Isome iliyoanzishwa mwaka 1976 mpaka sasa ikiwa na vyumba vinne vya madarasa.
Tabasam amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kumtuma Waziri mkuu au Makamu wa Rais kufika Sengerema kujionea wizi wa fedha za umma uliofanywa na watendaji wa serikali,huku akitumia nafasi hiyo kuwaonya madiwani wanaomjadili kwenye mitandao ya kijamii.