MOROGORO; VURUGU GARI LA CHOMWA MOTO,PIKIPIKI TATU WATU 20 WANUSURIKA KIFO MKOANI HUMO.

0

 

Watu sita wanashikiliwa na Polisi Morogoro kwa tuhuma za kuchoma moto mali mbalimbali za Serikali ikiwemo Gari moja aina ya Land Cruiser, pikipiki tatu, kifaa cha kupimia mipaka ya shamba na laptop 3.


Kamanda wa Polisi Morogoro Fortunatus Musilimu amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Melela kata ya Chita wilaya ya Kilombero ambapo Watuhumiwa walifanya hivyo wakati Maafisa ardhi walipofika katika shamba hilo ili kuhakiki mipaka yake baada ya kutokea migogoro ambapo ni shamba lenye ukubwa wa eka elfu mbili lenye umiliki wa Marehemu Daudi Balali ambaye alikua Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.


Musilimu amesema Mwekezaji huyo alipewa shamba hilo mwaka 2001 na Wanakijiji kwa makubalino ya kuwajengea Zahanati, Shule na kuwapatia huduma ya maji lakini hadi sasa makubalino hayo hayakuwa yametekelezwa ndio maana Wananchi wanalihitaji shamba hilo ili walifanyie shughuli za maendeleo.

Soma hii.NJOMBE,WANANCHI WAITAKA OPERESHENI SAKA WANAOTUPA WATOTO

Amesema katika tukio hilo Mtu mmoja amejeruhiwa ambaye ni dereva wa gari Damas Sanga( 51) baada ya Wananchi hao kumkuta kwenye gari hilo kisha kumshambulia sehemu  mbalimbali za mwili wake.

Watu zaidi ya 20 wakiwemo Watumishi watatu wa Wizara ya Ardhi wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na Wafanyakazi wa Wavamizi wa shamba la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Marehemu Daudi Balali ambapo shambulio hili lilitokea wakati wakiendelea na zoezi la upimaji wa shamba hilo ambalo kwa sasa linamilikiwa na Familia ya Balali katika Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero

 

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa Morogoro Frank Minzikuntwe amesema vurugu hizo  zimetokea baada ya maamuzi ya Serikali ya kulipima eneo hilo ili liweze kupangwa upya  baada ya kutelekezwa kwa muda mrefu huku Wananchi wanaolizunguka wakikosa maeneo ya kilimo.

Kamishna huyo amesema hali za Watumishi pamoja na Wananchi wengine zinaendelea vizuri baada ya kufikishwa katika vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri  hiyo.


“Dereva aliokolewa na Bodaboda wa pale Kijijini huku nyuma wale Watu (Wafanyakazi wa Wavamizi) wakachoma gari, pikipiki tatu, vifaa vya upimaji, laptop tatu zilizokuwa kwenye gari na mali nyingine, Wataalamu kwa kushirikiana na Wajumbe na Mgambo walikimbia kutoka eneo la shamba na kujiokoa.

Read more>>>
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top