MWALIMU AUAWA NYUMBANI KWAKE!

0


Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Arkisi Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Kasi Salai (50) ameuawa na mtoto wake wa kumzaa John Ammi (20) baada ya kuombwa fedha za matumizi na kisha akamnyima.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP), Marrison Mwakyoma, akizungumza na Mwananchi digital leo Agosti 2, amesema tukio hilo limetokea jana Agosti mosi.


Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha tukio hilo ni mwalimu huyo kuombwa fedha na mtoto wake wa kumzaa ili afanye matumizi yake, akamnyima kisha akamuua.


Amesema kijana huyo baada ya kumuomba mama yake fedha za matumizi na mama yake kumwambia hana chochote alichukia.
“Baada ya mtoto huyo kunyimwa fedha na mama yake alimpiga kichwani na kitu butu kisha mwalimu huyo akafariki dunia papo hapo,” amesema Kamanda Mwakyoma.


Amesema polisi wanamshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi kabla ya kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka hayo ya mauaji ya mama yake mzazi.


Ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutojichukulia sheria mkononi na pindi kukitokea tatizo laa kifamilia ni vyema kusuluhisha kuliko kusababisha mauaji kwani siyo suluhisho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top