Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikiria Mabula Joseph Mkazi wa Inyala Halmashauri ya Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya Mzazi mwenzake baada ya kukasirishwa na kauli za Mwanamke huyo kuwa hataki kuendelea na mahusiano .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Urlich Matei amesema tukio hilo la mauji lilitokea Agost 10 Mwaka huu Katika Kata ya Inyala ambapo Mtuhumiwa Mabula Joseph (31)alikuwa na ugomvi yeye na Mzazi mwenzake,Jema Mela (36) unaodhaniwa kuwa ni wivu wa Kimapenzi ambao ulipelekea kutokea kwa mauaji hayo.
“Katika eneo hilo kulikutwa panga moja na kopo lenye mabaki ya sumu aliyojaribu kujiua Mtuhumiwa baada ya kumuua mwenzake ingawa hakufanikiwa kujiua”
soma hii! Msichana aiba simu ya boss kumhonga mpenza wake