MWINGINE TENA AMUUA MKEWE KWA RISASI

0

 


Mwanamume mwenye umri wa miaka 42 anadaiwa kumuua mkewe kabla ya kujiua nyumbani kwao katika Kaunti ya Kiambu.


Kulingana na taarifa ya polisi kuhusu tukio hilo, Jonathan Mukundi Gachunga, ambaye alikuwa na leseni ya kumiliki silaha, anadaiwa kumpiga risasi mkewe wa miaka 30 kichwani kabla ya kujiua kwa kutumia silaha hiyo hiyo.


Miili ya wawili hao haikuwa na uhai ilipatikana ndani ya chumba chao cha kulala ambacho kilikuwa kimefungwa kutoka ndani Jumanne jioni.

 Hii ilikuja baada ya rafiki wa Mukundi kuripoti katika kituo cha polisi cha Kiambu mwendo wa saa kumi na mbili jioni kwamba marehemu hakuwa akipokea simu zake ambazo zilikuwa za kutiliwa shaka.

Wanandoa waliokutwa na umauti.


"Pamoja na maafisa wa kituo cha polisi cha Kiambu walielekea nyumbani kwake ambapo chumba cha kulala kilikuwa kimefungwa kwa ndani.

Kisha Mlango ulivunjwa ambapo miili ya Jonathan Mukundi Gachunga mkaazi wa Kikikuyu mwenye umri wa miaka 42 na mkewe ambaye ni Phelomena Njeri mwenye umri wa karibu miaka 30 walipatikana wakiwa hawana uhai, ”ilisema ripoti ya polisi.


Miili ya marehemu ilihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta ikisubiri uchunguzi.


Polisi walipata bunduki ndogo kutoka kwa tukio hilo. Sababu ya tukio hilo haikuweza kubainika mara moja.Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top