MZEE WA MIAKA 69 ABUNI WINCHI MKOANI NJOMBE,SHUHUDIA UZINDUZI WAKE!

0


Mzee Abubakar Isumael Msigwa(69) mkazi wa Njombe mjini amevumbua mtambo wa kunyanyua vitu vizito(Winchi) na kuitaka serikali kuona namna ya kumshika mkono katika jitihada zake za kubuni na kuvumbua mitambo ambayo inakwenda kuwapunguzia changamoto ya utenda kazi watanzania.


Akizumzia ubunifu mzee Msigwa amesema imemchukua miaka miwili na nusu kuvumbua mtambo huo huku lengo kuu likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya uchumi wa viwanda na kwamba ili kufikia lengo lake la kuwasaidia watanzania kiteknolojia ,anaomba serikali imuwezeshe vifaa ili akamilishe ubunifu wa mashine ya kubangua korosho mashine ya kuvuta maji zaidi ya km 20.


Awali wakitoa maoni kuhusu ubunifu huo baadhi ya viongozi wa kiroho waliofika kushughudia uwezo wa mtambo huo wakati ukifanyiwa majaribio ya kunyanyua magogo yenye uzito wa zaidi ya tani moja akiwemo Mchungaji Alphonce Ngavatula kutoka KKKT na Mchungaji Joseph Mtweve kutoka Mlima wa Faraja wamesema karama hiyo haipaswi kupotea kirahisi hivyo serikali ione umuhimu wa kumlinda na kusaidia mzee huyo.

Nao baadhi ya wakazi wa mji wa Njombe ambao wamekuwa wakiunga mkono jitihada za mzee Msigwa akiwemo Frank Msuya na kijana Peter Kayombo wanasema teknolojia ya mzee huyo iboreshwe zaidi ili mitambo hiyo ianze kuzalishwa nchini badala ya kutumia fedha nyingi kununua mataifa yaliyoendelea.

Mbali na mtambo huo,Mzee huyu pia alibuni mashine ya kupanda na kuvuna mazao miaka ya 1980 iliyomfanya hayati Mwalimu Nyerere kulazimika kukutana nae
Tazama video take hapa!


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top