NJOMBE;WANANCHI WAITAKA SERIKALI KUFANYA OPERESHENI SAKA WANAOTUPA WATOTO

0

 

kata hiyo kutoka vijiji vya Nyombo na Matiganjola wameita serikali kufanya operesheni madhubuti ya kuwasaka wazazi wanaotelekeza watoto kwasababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na migogoro ya kimahusiano na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao ili kukomesha vitendo hivyo.


Katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Lupembe wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kueleza mipango ya maendeleo, wakazi wa vijiji vya Matiganjola na Nyombo akiwemo Michael Salingwa na Grace Nyagawa wamesema katika vijiji vyao kumekuwa na vitendo vya kujirudia vya kutupwa na kutelekezwa watoto hivyo wanaomba nguvu ya ziada ichukuliw ya kukomesha vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa taifa la kesho.

Mbali na watoto wakazi hao pia wamezungumzia changamoto ya ongezeko la tozo za mbao na mkaa na kwamba serikali ipunguze ili kunusuru tatizo la kukimbiwa na wanunuzi wa malighafi hizo.

Soma hii MKE ATUHUMIWA KUMUUA MUMEWE 

Awali Mtendaji wa kata ya Ikuna Alestadia Naza na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Njombe Kasanga Makweta wanaswema kinachofanywa na baadhi ya wazazi kijiji hapo kina athari kubwa kwa vizazi vijavyo na kwamba chama hakitafumbia macho vitendo hivyo.

Nae mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swalle akitolea ufafanuzi wa kero mbalimbali zilizowarishwa amesema kutupa mtoto kunapoka haki za msingi za mtoto ikiwemo ya kuishi na kuagiza kudhibitiwa mara moja huku pia akisema kuhusu suala la kero ya ongezeko la tozo za mbao na mkaa atazisemea katika vikao vya bunge.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top