NYUMBA 19 ZA WANANCHI ZATEKETEA KWA MOTO PWANI

0

 

Picha za moja ya nyumba iliyoteketea kwa moto

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya ya Rufiji wamefika kwenye tukio la moto lililotokea usiku wa kuamkia leo 

Viongozi was wilaya na mkoa wamefika li kuona athari iliyotokea na jitihada ambazo uongozi wa wilaya wamezichukua kuhakikisha wananchi wanakuwa salama katika kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage Kata ya Mbwara ambapo nyumba zaidi 19 zimeteketea mara baada ya mwananchi mmoja akiwa anasafisha eneo lake moto ulimshinda na kuteketeza nyumba zipatazo 19 za wananchi pamoja na mali na thamani zilizopo ndani ya nyumba hizo na hakuna majeruhi yoyote katika ajali hiyo.

SOMA HII:- KURASA ZA MAGAZETI HII LEO AGOSTI 30 2021

Aidha Abubakari Kunenge ametoa pole kwa serikali ya wilaya pamoja na wananchi waliokutwa na madhira hayo na kuwapongeza wakazi wa maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi wananchi wenzao waliokutwa na ajali hiyo na kuwaagiza  uongozi wa wilaya hiyo kufanya haraka kujua tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo.


Kwa upande wake Mkuu wa wailaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameeleza kama wilaya hatua walizochukua mara baada ya kutokea tukio hilo na kutoa rai kwa wakazi wa wilaya hiyo kuw a makini wakati wanachoma moto kwani kwa sasa ni kipindi cha upep mkali.

Wananchi wa eneo hilo nao wameeleza tukio jinsi lilivyowaathiri hivyo kuomba serikali kuweza kuwasaidia kwa haraka maana hawana mahala pakuishi.

Read more>>>>>>

Nyumba iliyoteketea kwa moto


Mkuu wa mkoa wa Pwani akikagua nyumba hizo


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top