Hizi ni kauli za Rais Samia Suluhu Hassan leo akizindua kikao kazi cha Maaafisa Wakuu Waandamizi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa Jijini Dar es salaam.
1
“Tupo hapa kuhudumia Watu na sio kudidimiza Watu, Mshutumiwa anapokufa mikononi kwako Askari wa Polisi, umemchukua huko, umemburuzu, umeshamchapa virungu vya kutosha, Wanadamu tupo wa Afya tofauti mwingine unamchapa sana bado yupo ngangari, mwingine vifimbo viwili tu tayari amefariki,
2
“Nadhani matumizi makubwa ya nguvu IGP na yenyewe muyatazame, kesi za kufa Watu kwenye Vituo vya Polisi hazileti sifa nzuri kwa Serikali, nawaomba sana tendeni yaliyo haki”
3
“Yai viza lile yai bovu kwenye mayai mazima harufu yake hutapakaa zaidi kuliko yale mazima, kwenye Jeshi la Polisi wakiwepo wachache wenye tabia za ajabu sifa zake zinatapakaa kuliko mazuri”———Rais Samia
4
“kuchelewesha kwa upelelezi kunaongeza mzigo mkubwa kwa Serikali kuwaweka Mahabusu Jela, takwimu mpaka Mwezi huu tarehe 22 idadi ya Mahabusu katika Jela zetu ni karibu sawasawa na Wafungwa katika Jela zetu, Wafungwa walikuwa 16,542 lakini Mahabusu ni 15,194 mpaka juzi”
5
“Mahabusu hawa kuna waliokaa wiki, mwezi, mwaka na kila anayeguswa upelelezi haujakamilika, nitoe wito kwa zile kesi ambazo mna uhakika upelelezi hautokamilika basi watolewe wakafaidi Uhuru wao na zile kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi uharakishwe”
6
“Naomba mkae na Wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha Sheria za kuweka Watu Mahabusu, kwenye Nchi za wenzetu Mtu hakamatwi mpaka upelelezi umetimia akikamatwa anawekwa Mahabusu siku tatu nne tayari Mahakamani anahukumiwa anaendelea, huwezi kukuta Serikali inabeba mzigo wa Mahabusu kwa Maelfu, upelelezi haujakamilika”
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amezindua kikao kazi cha Maaafisa Wakuu Waandamizi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa Jijini Dar es salaam na kuzungumzia mambo mbalimbali kwenye Idara ya Polisi ikiwemo Ujambazi na uadilifu unaopaswa kuendelezwa na Polisi wote Tanzania.
8
“Wakati nilipoingia Watu walijaribujaribu, nilipoonana nanyi kule Kurasini nikasema kama mliweza kule nyuma siwaelewi kwanini leo msiweze, kauli yangu ile ilitoa changamoto na nawashukuru Leo Dar es salaaam ipo kimya, tunasikia kesi mojamoja mikoani na niwaombe wa Mikoani kafanyeni kila inavyowezekana Nchi ibaki salama, Nchi hii iepukane na vitendo vya ingang’anyi na Ujambazi” ———Rais Samia.
9
“Makosa ya jinai yamepungua kutoka 56,367 mwaka 2019/2020 hadi 49,508 mwaka 2020/2021 ukipiga mahesabu ya Watanzania tunaokisiwa kufikia Mil 60, tuseme Watanzania 40,000 wana uwezo wa kutenda makosa kwahiyo ukichukua idadi ya makosa na wanaoweza kutenda makosa unapata 0.00%, kwahiyo Tanzania makosa yapo kiwango cha chini hongereni sana Polisi” ———Rais Samia.