SHAKA: CHADEMA HAWAFANYI UTAFITI, WANGEKUWA WANAFANYA WANGEGUNDUA KIPAUMBELE NAMBA MOJA NI UCHUMI SIO KATIBA MPYA

0


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uwezo wa viongozi na makada wa chama hicho unatokana na utayari, uthubutu na kuujua umma unataka nini, kwa wakati upi na namna ya kutimiza mahitaji husika kulingana na changamoto zinazowakabili wananchi.


Pia kimesema chama cha siasa ambacho hakiwezi kuheshimu matakwa ya wanachama,  wananchi na Taifa  hutanguliza maslahi binafsi ya viongozi kuliko maslahi mapana ya umma kama wafanyavyo upinzani na hapo ndipo penye tofauti kati yao na chama tawala.


Hayo yamesemwa leo na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu  Shaka alipoulizwa iwapo CCM ina utofauti na upinzani alisema kuna utofauti kati ya viongozi wake na upinzani vivyo hivyo katika ubora wa muundo na sera CCM huwezi kukifananisha na chama chochote nchini.

Soma hii MAGAZETI YALIVYOANDIKA KUHUSU RAIS SAMIA,UHURU LAPOTOSHA UMMA

Shaka alisema kwanza vyama  upinzani hivyo  ukiacha kuwa ni vichanga, havijawa na uzoefu wa kutosha, viongozi  wake wamepatikana nje ya mifumo yenye kuaminika kwa jamii ikiwemo kutokimbazana na mahitaji ya wakati.


Alisema  mfano chadema iwapo kingelikuwa kinafanya tathmini au tafiti za kisiasa toka kwa wanachama wake na makundi mengine ndani ya umma kutaka kufahamu ajenda  ipi ni kipaumbele kwa wakati huu kati ya uchumi na katiba mpya, basi takwimu zingewaonesha kipaumbele namba moja ni uchumi.


Katika hili tunawakumbusha wakafanye rejea kwenye utafiti wa TWAWEZA sauti za wananchi ambao ulionesha vipaumbele vya wananchi na katika hivyo katiba haikuwepo, wananchi walitaja maji, afya, elimu, rushwa, miundombinu na uchumi. 


Alisema kutokana na chama hicho (Chadema) kushindwa kufanya  tafiti za msingi zenye kwenda sanjari na mahitaji ya wakati, ndiyo  maana kila wakati  kimekuwa kikijikuta kikishindana na nguvu za upepo kwa mujibu wa  wakati ndio maana hakijui kama uchumi wa watu ni kipaumbele cha kwanza na vingine hufuata baadaye.


"Chama bora na makini hujikita katika tafiti za kitaalamu kila mara ili kuweza kufahamu mahitaji ya wananchi na Taifa pamoja na namna nzuri ya kuyakamilisha.  Matakwa na mahitaji ya wakati yanapopishana na kuanza kuchomoza  ukaidi wa viongozi ni dosari na kiashiria" amesema Shaka

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top