WATU saba, wakiwamo askari polisi wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Bugarama kwa tuhuma za kutorosha mawe matatu yanayosadikiwa kuwa na dhahabu.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bulyanhulu, Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Abdalah Kombo, amesema jana kuwa watu hao walikamatwa juzi majira ya saa sita usiku.
Amesema kuwa askari polisi na baadhi ya wachimbaji wa madini walikamatwa kwa tuhuma hizo.
“Ni kweli tukio hilo lipo, askari polisi na baadhi ya wachimbaji akiwamo meneja wa mgodi wanashikiliwa kwa kosa la kutorosha dhahabu lakini nisiwe msemaji sana, taratibu za kipolisi zinaendelea, itakapodhibitika, hatua za kisheria zitachukuliwa," amesema.
Chanzo; Nipashe