SONGWE: WANANCHI TUMECHOSHWA NA ADHABU YA VIBOKO NA MCHANGA

0


Wananchi wa kata ya Itumba Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wametishia kumsusia shule ya sekondari Itumba afisa elimu sekondari wa wilaya kwa madai ya  kushindwa  kudhibiti adhabu ya viboko na uchimbaji wa mchanga inayotolewa na walimu wa shule hiyo kwa wanafunzi wanapokosea.


Wananchi wa kata ya Itumba wakiongozwa na diwani wa kata hiyo mbele ya mbunge wa jimbo la Ileje ambaye  pia ni naibu waziri wa ujenzi  Godfrey Kasekenya wamesema changamoto ya adhabu kwa wanafunzi  imekuwa kero kubwa kwa wazazi ingawa wamejaribu kuwaita walimu wa shule hiyo kwenye vikao vya maendeleo ya kata bila mafanikio.


Afisa elimu sekondari wilaya ya Ileje Grolia  Kangoma akijibu tuma hizo  amekiri kuwepo kwa suala la wanafunzi kubeba mchanga na mawe na kusema kuwani kwa  nia njema ambapo  mpaka sasa jambo hilo limestishwa huku akielezea kufatilia tuhuma za walimu kuwachapa viboko wanafunzi.


Kwa upande wake mbunge wa Ileje Mhandisi Kasekenya baada ya sikiliza kero amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kufatilia changamoto hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top