TABORA;ATUHUMIWA KUMUUA ALIYEMUOA MTALAKA WAKE!

0

 Mkazi wa Kijiji Cha Nyangahe, kitongoji cha Lungu ,wilayani Uyui, Mhonyiwa Mwanagwalila. anatuhumiwa kumuua Mgogo Gwahendwa ambaye alimuoa mke aliyemuacha.


Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatano Agosti 11, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Safia Jongo,amesema tukio hilo limetokea jana katika katika kata ya Bukumbi wilayani Uyui.

Amesema marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine hali iliyomfanya mtuhumiwa apate wivu na hivyo kuamua kumvizia mwanaume aliyemuoa mkewe akiwa njiani na kumuua.

Soma hii WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUCHOMA MOTO NYUMBA NA MTOTO MCHANGA

Kamanda Jongo amesema mtuhumiwa alikuwa na wenzake ambao baada ya kufanya mauaji hayo hawakuchukua chochote licha ya marehemu kuwa na Sh 200,000 na baiskeli.

Kwa mujibu wa kamanda Jongo,mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kufanya mauaji, akidai kulipiza kisasi kwa kumuua aliyemuoa aliyekuwa mkewe.

Diwani wa kata ya Bukumbi, James January,amesema marehemu aliwahi kufumaniwa mara mbili na mtuhumiwa na baadae aliamua kumuoa mwanamke huyo baada ya kuachwa.

Mkoa wa Tabora unakabiliwa na matukio ya mauaji yanayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi,imani za kishirikina na ulipaji visasi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top