(TIN) NUMBER TRA SASA NI BURE

0

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla amezindua kampeni ya usajili wa Walipakodi wapya ikiwa ni utekelezaji wa wa Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya kuitaka TRA kutanua wigo wa ukusanyaji wa Kodi.RC Makalla ametoa wito kwa Wafanyabiashara ambao bado hawajasajili biashara zao kuzisajili ili waweze kutambulika na kutimiza takwa la kisheria la ulipaji wa kodi.


Makalla amewataka Wafanyabiashara kutunza kumbukumbu ili kurahisisha zoezi la ukadiriaji na ukusanyaji wa kodi na kuwasisitiza kutoa risiti wanapouza na Wananchi kudai risiti.


RC Makalla ameonesha pia kuchukizwa na tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia Wamachinga kukwepa kodi na kuikosesha Serikali mapato.


Zoezi la usajili Walipakodi wapya limezinduliwa Mkoa wa Dar es salaam na litatekelezwa Nchi nzima ambapo TRA itakuwa ikitoa namba ya Utambulisho wa mlipakodi (TIN) bure pamoja na Tax clearence kwa Wafanyabiashara wapya lengo likiwa ni kuongeza mapato.Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top