VYUMBA VYA MADARASA VYAMCHEFUA WAZIRI UMMY AKIWA ZIARANI!

0

 Waziri wa TAMISEMI Mhe.Ummy mwalimu amewanyooshea kidole Uongozi wa Halmashauri ya Sengerema kwa kwashindwa kuweka vipaumbele kwenye Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.Waziri Ummy akiwa ziarani Wilayani Sengerama mapema Tarehe 14.08.2021 alibaini baadhi ya changamoto kwenye maeneo mbalimbali ambayo kama Halmashauri wangeweka vipaumbele changamoto hizozingeshatatuliwa.


Waziri Ummy alitembelea Shule ya Msingi Sengerema Kata ya Nyampulikano kukagua matundu ya vyoo ambayo ni chakavu kwa muda mrefu na pia sio salama kwa watoto pamoja na Shule ya Msingi Isome ambapo alijionea namna watoto wanasomea kwenye vyumba ambavyo havina Sakafu na uhaba wa madawati.


Aliwahoji Watumishi wa Halmashauri hiyo kwanini changamoto za namna hiyo ambazo zinagharimu fedha ndogo tu hazijatatuliwa kwa muda mrefu ilihali Halmashauri unakusanya mapato ya kutosha.


“Changamoto ninayoiona hapa Viongozi wa Halmashauri hamna vipaumbele vinavyoeleweka kama kuweka sakafu Darasa moja haiwezi kuzidi hata Laki sita ina maana halmashauri mmeshindwa na kuacha watoto wasome kwenye darasa hili na wakae chini kwa kukosa dawati wakato dawati moja ni sh elf hamsini? Alihoji Waziri Ummy


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top