WAZIRI ATOA MAAGIZO MATATU KWA WAKURUGENZI

0Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe Ummy Mwalimu amesema Uchambuzi wa awali wa Uteuzi wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan unaonyesha kuwa Wakurugenzi 70 wamehamishwa vituo vyao vya kazi na Wakurugenzi 45 wameendelea kuwepo kwenye vituo vyao vya kazi.


Akizungumza na Waandishi wa Habari  Mhe. Ummy  amebainisha kuwa Wakurugenzi 69 ni wapya  kati ya hao Wakurugenzi 15 wamejaza nafasi zulizokuwa wazi na Wakurugenzi 54 wamechukua nafasi za Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa.


Aidha Waziri Ummy pia amebainisha kuwa Uchambuzi wa awali unaonyesha kati ya Wakurugenzi wapya 69 wanawake ni 33 sawa na asilimia 48 hivyo kufanya idadi ya Wakurugenzi wanawake kuwa 55 sawa na asilimia 29 ya Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Maelekezo ya Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu kwa Wakurugenzi Wateule wa Mamlaka za Serijali za Mitaa I. Wakurugenzi wote wateule wakaripoti kwenye vituo vyao vya kazi ndani ya siku tano kuanzia Tarehe 03.08.2021 na makabidhiano ya ofisi yafanyike mara moja.


ii. Wakurugenzi ambao majina yao yameonekana kutokea kwenye maeneo zaidi ya moja wataripoti kwenye kituo ambacho jina limeonekana kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya uteuzi. Aidha, pale palipojirudia jina patatambulika kama nafasi wazi na itajazwa hapo baadae. (Nafasi hizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na Halmashauri ya Mji wa Njombe). 


iii. Wakurugenzi ambao uteuzi wao umesitishwa wakaripoti kwa Makatibu Tawala na Makatibu Tawala wa Mikoa wawapokee na kuwapangia majukumu @ummymwalimu


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top