ASKARI AKAMATWA AKIJINYONGA!

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linamshikilia askari wa Jeshi la Magereza mwenye namba B 9780 WDR Said Hassan Said (26) , Mkazi wa Ukonga kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 29 (jina linahifadhiwa).

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokea Septemba 1,2021 majira ya saa tano nusu usiku katika barabara ya madafu Ukonga jijini Dar es salaam.

SOMA HII>TAZAMA JEZI ZA SIMBA SC ZILIZOTAMBULISHWA LEO

"Mtuhumiwa huyo ambaye ni askari wa Jeshi la Magereza mwenye namba B 9780 WDR Said Hassan akiwa na mwenzake ambaye bado hajakamatwa walimkamata kwa nguvu msichana huyo na kumuingiza kwenye gari dogo kisha kuondoka naye hadi kwenye nyumba moja iliyopo karibu na kambi ya KMKM Ukonga Magereza na kuanza kumbaka na kumlawiti kwa zamu", ameeleza Kamanda Magiligimba.


"Baada ya kumaliza kumbaka na kumlawiti watuhumiwa hao waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kumsababishia majeraha makubwa na maumivu makali katika sehehmu zake za siri",ameongeza Kamanda Magiligimba.


Amefafanua kuwa baada ya mtuhumiwa kugundua kuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tukio baya alilolifanya na mwenzake, mnamo tarehe 02/09/2021 alijaribu kujiua kwa kujinyonga na kuacha ujumbe wa maandishi kwa mkuu wake wa kazi na askari wenzake kuwa “mnisamehe bure kwa uamuzi wangu niliochukua kwa tukio nililolifanya nitaonekana nimekufa kizembe”.


Hata hivyo kabla mtuhumiwa huyo hajafanikisha azma yake ya kujitoa uhai alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi.


"Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linaendelea na msako mkali kwa mtuhumiwa mwenzake aliyekimbia baada ya tukio hilo baya na linamtaka ajisalimishe haraka iwezekanavyo katika kituo chochote cha Polisi",amesema Kamanda Magiligimba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top