WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI,

0

 


Mwandishi wa habari wa Global TV, ambaye kituo chake cha kazi ni jijini Dodoma, Mohamed Zengwa (pichani chini) na wenzake wawili wamepata ajali mbaya ya gari Jumanne, Septemba 21, 2021 katika Kijiji cha Usimba, wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

Zengwa na wenzake akiwemo dereva wa gari hilo na mwanahabari wa Dar Mpya, John Marwa, wamepata ajali hiyo baada ya gari aina ya Land Cruiser V8 lenye namba za usajili T 835 DRR walilokuwa wakilitumia kupasuka tairi ya nyuma na ya mbele ya upande wa kushoto na kusababisha gari hilo kupoteza uelekeo na kupinduka.

Watu wote watatu waliokuwa kwenye gari hiyo, hawajaumia sana zaidi ya kupata majeraha madogo madogo na hali zao zinaendelea vizuri ambapo wamekwenda hospitali kwa ajili ya vipimo matibabu zaidi.

Zengwa na wenzake hao, walikuwa wakisafiri kuelekea mkoani Kigoma kikazi.

Uongozi na wafanyakazi wote wa Global Publishers Ltd, tunawapa pole ndugu zetu hawa kwa ajali hiyo, pia tunamshukuru Mungu kwa kuwanusuru kutokana na ajali hiyo mbaya na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye majeraha waliyoyapata ili warejee kuungana na familia zao na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

CHANZO - GP

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top