Polisi wamemkamata mhudumu mmoja wa hoteli baada ya wanaume wawili waliokuwa wanatafuta penzi lake kupigana ndani ya nyumba yake na mmoja wao kufariki dunia.
Katika kisa hicho kilichotokea mtaani Mwiki, Nairobi,nchini Kenya mwanaume mmoja asiyejulikana aliangamiza maisha ya David Maina, 35, wakimpigania Miriam Njeri mwenye umri wa miaka 27.
Kama ilivyoripotiwa na The Standard, Njeri akiwa ameandamana na Maina walikuwa wakirejea nyumbani kwake mwendo wa saa saba na dakika 40 usiku wakitokea eneo la burudani kujiburudisha na vinywaji.
Hata hivyo, wakati walifika kwenye nyumba, walimpata mwanaume mwingine akisubiri kufaidi penzi la Miriam na ndipo vita vikaanza.
Vita hivyo vilivyoanza kwa maneno viligeuka kuwa vya mangumi na mateke ambapo jamaa aliyekuwa na hasira alimpiga Maina na jiwe kichwani na kumuua papo hapo.
Kachero wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Kasarani, Vincent Kipkorir alisema mshukiwa aliingia mitini baada ya kutambua ameua.
Kisha Njeri alikamatwa na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kasarani ili kusaidia katika uchunguzi.
Msako wa mwanaume huyo imeanzishwa.
Chanzo - Tuko News