Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la GOERGE MICHAEL anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 45 mkulima na mkazi wa kitongoji cha Mnadan kata ya Mchikichini Wilayani Urambo amekutwa amejinyonga nje ya nyumba yake asubuhi huku chanzo Cha kajinyonga kwake hakijajulikana
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnadani Seligius Mkulila amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Diwani wa kata ya Mchikichini ATHUMAN MWINIKO amesema kuwa matukio ya kujinyonga yamekuwa mengi na kuwasisitiza wnanachi wa kata kutokuwa wasiri katika mambo yanayowatatiza.
Marehemu ameacha mke na watoto wanane ambapo tukio hilo linafanya kuwa tukio la 9 kuripotiwa na @cgfmradio la mtu kujinyonga Wilayani Urambo kuanzia January hadi Oktoba ambapo mwezi uliopita aliripotiwa mwanaume mwingine kujinyonga katika kijiji cha moto moto kata ya vumilia jirani na kijiji hicho.