Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania leo kumuamuru Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba kumlipa Bernard Membe Tsh. Bilioni 6 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari, Wakili Shundu Mrutu amejibu maswali ya wengi waliotaka kufahamu sheria inasemaje iwapo Musiba atashindwa kulipa pesa hizo.
"Sheria baada ya kutoka kwa hukumu Musiba asipofanya hivyo sheria imeweka namna ya kumlazimisha kulipa fedha hizo, aliyeshinda anaweza kuomba Mahakama imsaidie kumlazimisha Musiba alipe fedha hizo na moja wapo ya njia ni kukamata mali zake na kuziuza ili zifidie, ikishindikana........ njia nyingine ni (Membe) anaweza kuiomba Mahakama Musiba akamatwe na afungwe kama Mfungwa wa madai kipindi cha miezi sitasita mpaka pale atakapolipa fedha hiyo" ——— Wakili Shundu Mrutu.