KWANINI MKURUGENZI WA MASHTAKA HUFUTA MASHTAKA au KESI?

0

Bila shaka umekuwa ukisikia kuhusu mkurugenzi Wa Mashtaka amefuta kesi Fulani,lakini huenda huwa unajiuliza kwanini afute kesi,ni wakati gani Wa kufuta kesi/Mashtaka Je! Sheria inampa uhalali huo kwa sheria IPI?.


Ungana na Jungu LA Sheria Tanzania kufaham hili.👇👇

KIFUNGU CHA 91(1) CHA SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI, SURA YA 29 ILIYOREJEWA 2019,  KINASEMA:;


Katika kesi yoyote ya jinai na katika hatua yoyote ile kabla ya hukumu au uamuzi, kama itakavyokuwa, Mkurugenzi wa Mashtaka anaweza kufuta kesi aidha kwa kueleza mahakamani au kwa kuiambia mahakama husika kwa maandishi kwa niaba ya Jamhuri kuwa mwenendo hautaendelea;


Na baada ya hapo mtuhumiwa ataachiwa mara moja kuhusiana na shtaka ambalo limefutwa na kama amepelekwa gerezani atatakiwa kuachiwa, au kama yuko chini ya dhamana wadhamini wake watakoma kuwa wadhamini; 


Lakini kuachiwa huko kwa mtuhumiwa hakutachukuliwa kama kizuizi kwa mashtaka mengine ya baadaye dhidi yake kwa kutumia maelezo hayo hayo.


Kifungu kidogo cha pili cha kifungu cha 91 kinaelekeza kwamba, iwapo mtuhumiwa hayupo mbele ya mahakama wakati shtaka lake linafutwa, msajili au karani wa mahakama atatakiwa mara moja kuhakikisha notisi ya maandishi ya kufutwa kwa kesi inapelekwa kwa mtunzaji wa gereza ambamo mtuhumiwa anaweza kuwa anazuiwa na kama mtuhumiwa amepelekwa kwa kusikiliza shauri, kwa mahakama ya chini ambako ndiko alikosikilizwa na mahakama hiyo italazimika mara moja kuhakikisha notisi kama hiyo ya maandishi anapewa shahidi yeyote anayewajibika kutoa ushahidi na kwa wadhamini wake (kama wapo) na vilevile kwa mtuhumiwa na wadhamini wake kama alishatolewa kwa dhamana.

Usikose fundisho lijalo kuhusu sheria!

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top