MAMA ATUHUMIWA KUTUPA KICHANGA CHA SIKU TATU!

0

 #HABARI JESHI la Polisi mkoani Mbeya, limemkamata Janeth Peter (32), Mkazi wa Kiwira wilayani Rungwe kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mwenye umri wa siku tatu, jinsia ya kike, ambaye baadae alikutwa na wasamaria wema akiwa amefariki.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema,  mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 20,2021 majira ya saa moja usiku baada ya polisi kufanya msako mkali katika Kata ya Kiwira  na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo.


Kamanda Matei amesema hadi wanaendelea kumhoji  pamoja na uchunguzi wa kitabibu kwa kushirikiana na wataalam wa afya ili kufahamu endapo alitoa mimba au ana matatizo ya kiafya sambamba na kufahamu sababu ya kufanya tukio hilo la kinyama  na kwamba baada ya upelelezi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.


Ikumbukwe kuwa Oktoba 20,2021 majira ya saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Makaburini Kata ya Kiwira mwili wa mtoto mchanga ulikutwa ndani ya shimo la choo kilichopo nyumbani kwa Salome Lutengano (36) na ndipo jitihada za kuutoa zilianza lakini tayari alikuwa amefariki dunia.Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top