Leo katika kona ya sheria Karibu tena tukufahmishe hili la UWAKALA WA UKAHABA na adhabu yake!.
KIFUNGU CHA 139 KANUNI YA ADHABU SURA YA 16.
Mtu yeyote ambaye- (a) analeta au anajaribu kuleta mtu yeyote, ikiwa ni mwanamke au mwanaume wa umri wowote, kwa idhini au bila ya idhini yake kuwa kahaba, ndani ya Jamhuri ya Muungano au nje ya Jamhuri ya Muungano;
Anamsababisha, au anajaribu kusababisha mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane, kuondoka katika Jamhuri ya Muungano, au bila ya ridhaa ikiwa ni kwa au bila ya idhini ya mtu huyo, au bila ya idhini kwa nia ya kumsaidia ajihusishe na ngono zisizo halali na mtu yeyote nje ya Jamhuri ya Muungano, au akimuondoa au kujaribu kumuondoa kutoka katika Jamhuri ya Muungano, mtu huyo, kwa ridhaa yake au bila ridhaa yake kwa nia hiyo;
Anasababisha, au kujaribu kusababisha, mtu yeyote wa umri wowote, kuondoka katika Jamhuri ya Muungano, kwa ridhaa au bila ridhaa yake, kwa nia ya kwamba mtu huyo atakuwa anaishi au anakwenda kwenye danguro, mahali popote au atamuondoa au kujaribu kumuondoa mtu huyo kutoka katika Jamhuri ya Muungano, kwa ridhaa au bila ridhaa yake kwa nia hiyo; anamleta, au anajaribu kumleta katika Jamhuri ya Muungano mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane kwa nia ya kumshirikisha kwenye ngono haramu na mtu yeyote hapa ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano;
Anasababisha, au anajaribu kusababisha mtu yeyote wa umri wowote, kwa ridhaa au bila ridhaa ya mtu huyo, kuondoka kwenye maskani yake anayoishi katika Jamhuri ya Muungano ambayo si danguro, kwa nia ya kumhusisha mtu huyo na ukahaba, kuishi au kuhudhuria mara kwa mara kwenye danguro, ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano;
Anamfungia mtu yeyote bila ridhaa ya mtu huyo kwenye danguro lolote au sehemu yoyote kwa nia ya kufanya ngono haramu au udhalilishaji wa ngono kwa mtu huyo, atakuwa ametenda kosa la ukuwadi na akipatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka kumi na kisichozidi miaka ishirini au faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shillingi laki tatu, au vyote kwa pamoja.