YAMENIKUTA; JIRANI YANGU ALIVYONIFANYA NIMUACHE MUME WANGU!

0

Sikuwahi kuwa na mazoea naye, ni Mama niliyekua nikimheshimu kwani mbali na kuwa alinizidi umri lakini alikua anatoka katika kabila letu hivyo mara nyingi nilipenda kumsalimia kwa heshima na aliniita mdogo wake. Kwakua siku ana mazoea naye sikua nikijua kuhusu Maisha yake, nilikua nikimuona tu peke yake basi bila kujua kama ana mwanaume au la, sikua nikimfuatilia kabisa.Wakati naenda kujifungua nilimuaga kwani kama nilivyosema ni mtu kutoka kabila letu, nilienda na kukaa miezi mitatu, mimi na mume wangu tulikua vizuuri tu, ananihudumia kwa kila kit una katika kipindi chote hicho sikuwahi kugombana naye kwa lolote. Lakini baada ya kurudi kila kitu kilibadilika, kwanza yule dada alianza kuleta mazoea, akawa karibu na mimi kunichimbachimba na kutaka kujua ni kwa namna gani nilikua nikiishi na mume wangu.


Mwanzo niliona kama kitu cha ajabu lakini kuna siku aliamu akuniambia.

“Mdogo wangu, nilipanga nisikuambie kwani niliona kama naingilia ndoa yako lakini wewe ni kama ndugu yangu, tunatoka sehemu moja, huyu mume wako ni sheteni, ni mnyama saa, wakati umeondoka kwenda kujigundua alikua akileta wanawake ndani. Yaani kila siku yeye alikua ni mtu wa kubadilisha wanawake, anamleta mwanamke wanalala naye anaondoka asubuhi na wala hajali kama watu wanaumipona. Kuna mwingine alikuja na kukaa hapa karibu wiki, huo ndiyo alikua anapika na kupakua.


Anakuja hapa, tena kidada kina dharau hicho, kuna siku niliamua kuuambia ukweli kuwa huyu mwanaume kaoa hivyo achana naye lakini badala ya kunielewa aliishia kunitukana na kuniambia nihangaike na ndoa yangu!” Yule dada aliniambia mambo mengi sana kuhusu mume wangu, aliniambia visa vingi mpaka kuchanganyikiwa, nilikua najua mume wangu ni mtu wa dini hanywi hata pombe lakini alinifungua maicho kwa kuniambia kuwa mume wangu ni mlevi sana tena wa kupindukia.


Nilijikuta nakasirika, kichwa kinaniuma. Aliniomba sana nisimuambie mume wangu bali nichunguze mwenyewe kwani yeye kaniambia kama ndugu yake na asingetaka kuonekana mnafiki. Nilimsikiliza na kukaa kimya, mume wangu alivyorudi sikumuambia kitu chochote, nilijikuta nakua na hasira, nimenuna simuambii kitu, nilianza kumchunguza mume wangu, kushika simu yake na kukagua kila namba, nilikuta mkweli anawasiliana na wanawake ambao hupigiana nao simu mara kwa mara lakini kila wakati nikiingia kwenye meseji zake nakuta zimefutwa, hakuna meseji kwenye hizo namba kitu ambacho kiliniaminisha kuwa anakua makini kwa kufuta meseji mili nisizione.


Hali hiyo ailinitesa sana, wiki nzima niliona kama mume wangu kabadilika, ikajikuta nakua na kisirani, tukawa tunagombana, nikawa nakasirika kasirika mambo  madogo, kila alichokua ananifanyia nilihisi mkama anaigiza, naye alikua mkali, akaanza kunijibu hovyo, sikumuambia kilichotokea lakini naye alijua kuwa sipo sawa ila kila aliponiuliza sikumuambia kitu chochote. Ghafla niliona kama Maisha yangu yamefika mwisho, mwanaume niliyempenda sikumuona kama mume tena, nilimuona kama adui hivyo sikuona sababu ya kuendele kuishi naye.


Siku moja mume wangu akiwa kazini nilichukua kila kitu kilichochangu, nikamchukua na mwanangu na kurudi nyumbani kwetu. Sikumuambia chochote, nilirudi nyumbani na waliponiuliza niliwaambia nimekuja kupumzika lakini sikuwaambia sababu.  Mumewa alinipigia sana simu lakini sikupokea, sikutaka kuongea naye, alimpigia Baba yangu simu aliyemuambia kuwa nipo nyumbani lakini sitaki kuzungumza.


Alikuja mpaka nyumbani ila sikumuambia sababu ya kuondoka, nilimuambia nahitaji kumlea mwanangu mbali kabisa nayeye, alibembeleza kujua sababu lakini sikumuambia, nilimuambia tu mimi sitaki kurudiana naye yeye aendelee na Maisha yake. Mama yake naye alinipigia simu lakini naye sikutaka kuongea naye, nilikua nahasita sana nikikumbuka Maisha niliyoanzia na mume wangu wakati tunalala chini hana hata kitanda basi niliona sisitahili kufanyiwa hivyo.


Wakati huo huo huyo dada alikua ananiambia mambo yaliyokua yanaendelea kwangu, mume wangu alikua anakuja kuniomba msamaha huku napata Habari kuwa kuna mwanamke mwingine naishi naye tena nyumbani kwangu, niliona kama ananidhihaki, nilikua napatwa na hasira nusu kuchanganyikiwa. Nilikaa nyumbani kwa miezi mitatu bila kupata muafaka, mume wangu alichoka kuomba msamaha na kutaka kujua sababu ya mimi kuondoka mwisho naye alikaa kimya bila kusema kitu chochote.


Alipunguza kunipa pesa za matumizi kitu ambacho kilinjifanya niamini kuwa kweli alikua kanichoka na ana mwanamke mwingine, nikaanza kudai talaka bila kuongea kitu chochote kwa mtu yoyote. Wakati wote huo huyo dada alikua karibu yangu, siku moja aliniambia kuwa yuko Morogoro kikazi hivyo anataka kuonana na mimi, siku ana hiyana kwani mimi kwetu Moro hivyo niliona kama shoga yangu kaja kinifariji.


Alikuja nyumbani nikamkaribisha vizuri, alikuja kweli kwenye semina hivyo nilimsihi sana kulala nyumbani kwetu kwani kwao ilikua ni nnje kidogo ya mji, mwanzo aligoma lakini baadaye alikubali. Usiku tuliongea mambo mengi sana, aliniambia kuwa mume wangu hanifai nahitaji kuendelea na Maisha yangu, ingawa bado nilikua nampenda mume wangu lakini kwa mambo aliyokua ananiambia yule dada niliona siku ana sababu ya kuendelea na ndoa yangu.


Usiku alikua ameenda kuoga, sumu yake aliweka ilianza kuita sikuhangaika nayo lakini wakati naisogeza pembeni ili isidondoke kwani ilikua na vibration meseji iliingia, siku ana mpango wa kuisoma lakini pale juu ilisomeka “Umeonana na mke wangu anasemaje….” Nilishangaa na kuhisi kama mimi, nilitaka kufungua lakini haikufunguka, niliigeuza chini ili sijue kama nimeiona lakini nilipata hamu ya kujua ni nani huyo alikua akimuuliza hivyo kwani namba ilikua imeseviwa “Bestiee”.


Nilisubiri aliporudi nikaangalia vizuri nikakariri pattern hivyo alivyolala usiku tu nilichukua simu yake, nikafungua nilichokutana nacho sikuamini macho yangu. Walianza kuchart siku niliyoondika nyumbani, huyu dada alionekana kumtafuta mume wangu na kumsalimia, walionekana kama hawana mazoea kwani kuna wakati mume wangu alimuuliza “Samahani wewe ni nani?” Huyo dada alijibu kwa kujitambulisha kuwa yeye ni nani na kumuambia kuwa ni Rafiki yangu na anajua kwanini nimeondoka.


Mume wangu hakuonekana kujali, hakujibu meseji zake kwa Zaidi ya wiki tatu mpaka alipokuja kuongea na mimi nikakataa kumuambia sababu ya mimi mkuondoka ndipo alimtafuta yule dada na kutaka kuongea naye, sikuona kitu kingine lakini ilionekana kama vile walionana na kuongea kwani baada ya hapo walionekana kuchart huku huyo dada akimuambia kuwa ananijua familia yetu si familia ya kuoa hivyo yuko tayari kumtafutia mwanamke mwingine ingawa mume wangu hakuwahi kumjibu kuhusu hilo.


Siku hiyo ni kama mume wangu alimtuma ili kuongea na mimi kunishawishi kurudi nyumbani lakini alikua anamkatisha tamaa, niliingia whatsapp nikakuta huyo Dada anamtumia mwanaume picha za mdogo wake na kumsisitiza kuwa ni mtu mwenye nidhamu, mume wangu aliishia kumsifia tu lakini hakutaka kabisa kuzungumzia kama amuunganishie au la? Nilijikuta natetemeka kwa hasira, nikaona namna anavyonipondea kwa mume wangu huku akiniambia na mimi niachane na mume wangu ataniua wakati huo yeye anampigia debe mdogo wake, nilijikuta nakasirika na kumuamsha.


Badala ya kujibu nilichokiona alinigeukia na kuanza kunitukana huku akiniambia kuwa ni tabia mbaya kushika simu yake, alikasirika na kuondoka usiku uleule, niligombana naye sana na hapo ndipo wazazi wangu walijua ni kwanini nilikua nimeondoka kwa mume wangu. Kila mtu alinishangaa kuwa niliondoka kwa kusikia maneno ya watu bila kumuuliza hata mume wangu kama kafanya kitu gani.


Nilimuamini jirani, siku iliyofuata nilimpigia simu mume wangu kumuomba msamaha huku nikimuambia kuhusu huyo dada na mambo aliyokua ameniambia. Mume wangu alinisikiliza sana lakini baadaye wakati nikihisi kama amenielewa na anakaribia kinisamehe aliniambia.

“Ninachotaka ni kupima DNA kujua kama huyo mtoto ni wangu au ni mtoto wa Hamisi! Yaani umefumaniwa huko ndipo unajifanya kutaka kurudi kwangu kwakua Malaya wako hataki kukuoa tena?” Nilihisi kuchanganyikiwa, Hamisi aliyekua anamzungumzia mume wangu ni Kaka mmoja ambaye nilitafutiwa na huyo Dada.


Baada ya kuondoka kwa mume wangu huyo Dada aliniambia kuwa kuna mkaka ananipedna hivi hivi na mwanangu na yupo tayari kunioa, ingawa sikua tayari kwa hilo lakini alinisihi sana kuonana naye na kumsikiliza. Kweli kuna siku nilitoka nae, nikaenda kuonana naye. Tuliongea sana lakini sikumuelewa. Pamoja na kwamba sikutaka kuwa naye kwenye mahusiano lakini alikua akinitumia meseji nyingi kuhusu mtoto, anajali na kuniambia yuko tayari kumlea.


Mimi nilikua namjibu tu kama anavyotaka lakini sikumkukubalia kimapenzi, kumbe zote zilikua ni njama za jirani kwani alimtumia screenshot za meseji ambazo namjibu vizuri Hamisi Pamoja na picha zetu Pamoja kwamba nilishaonana naye sehemu kama mara tatu na kuna siku alikuja mpaka nyumbani kumuona mtoto wangu, akapiga na picha, mimi nilijua anafanya hivyo kama Rafiki kumbe alikua anapiga picha na mwanangu na kuzipost katika mitandao kama ni mtoto wake ili tu kuniharibia, yule dada alimuonyesha mume wangu na usiku ule tulipogombana alimuwahi mume wangu


Hapo ndipo alimuonyesha picha za mimi na Hamisi, kurasa za Hamisi kwenye mitandao ya kijamii na meseji akamuambia kuwa, siku hiyo Hamisi aligundua kua kumbe nimeolewa na kuamua kuniacha, nilipomtafuta mume wangu kumuambia kuhusu huyo dada tayari alishampanga na hakutaka kunisikiliza.


Kama utani mume wangu alinipa talaka na kudai tupime DNA, kusema kweli nilichanganyikiwa kwani kwa hasira mume wangu aliamua kuoa mwanamke mwingine na kuanza kuishi naye. Tulisumbuana kuhusu DNA kwa mwaka mzima ndipo nikakubali tukapima mtoto alipoonekana ni wake basi akaanza kuhudumia, aligoma kabisa kunisamehe kwani mbali na DNA kuonyesha kuwa mtoto ni wake lakini bado alikua anaamini kuwa nilimsaliti na ndiyo ilikua sababu ya mimi kuondoka.


Nilikua na mawazo sana kiasi kwamba nikaja kuingia kwenye mahusiano na mume wa mtu, nikabeba ujauzito wake lakini kabla ya kujifungua aliniacha, mwaka jana mume wangu alijua ukweli kuwa yule Dada alimdanganya baada ya wao kugombana ndipo akamuambia ukweli kuwa alimdanganya ili kumharibia, mume wangu alirudi kwangu kuomba msamaha na kutaka turudiane lakini baada ya kujua kuwa nimezaa na  mume wa mtu aliniambia hapana, tuliachana mpaka sasa Maisha yangu hayaeleweki kwakua tu niliamua kumsikiliza jirani!

CREDIT ; IDD MAKENGO

MWISHO

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top