AFARIKI DUNIA KWA KUVAMIWA NA NYUKI AKIWA NYUMBANI KWAKE

0


Mkazi wa kijiji cha Rau River Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Mathias Mallya (75) amefariki dunia baada kushambuliwa na kundi la nyuki wakati akiwa nyumbani kwake.

Nyuki hao ambao walikuwa juu ya mti walimvamia mzee huyo baada ya tawi ambalo lilikuwa na sega kuanguka kutokana ya ngedere kutua kwenye tawi hilo.

Akizungumza na Mwananchi, Diwani wa Kahe, Aloyce Momburi amesema nyuki hao walimng’ata sehemu mbalimbali za mwili mzee huyo hali ambayo ilimpeleka kupoteza maisha.

"Hawa nyuki walikuwa kwenye mwembe, sasa ngedere alikuwa anapita akawa amerukia kwenye tawi lenye sega la nyuki ambapo lilikatika na kudondosha nyuki,"

"Huyu mzee alikuwa jirani na nyumbani kwake ikabidi asogee kuangalia ni nini kimetokea baada ya kuona nyuki wakizagaa kwa wingi alipoenda kuangalia nyuki wale wakaanza kumshambulia ikabidi akimbilie ndani bado wakamfuata na kuanza kumshambulia muda mchache aliishiwa nguvu na kupoteza maisha,"

Alisema jitihada za kumkimbiza hospitali hazikuzaa matunda kwani alikuwa ameshafariki na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Rau ya Kati, Michael Massawe amesema shughuli za kuondoa nyuki hao zimeanza kufanyika na tayari TFS wamefika kwa ajili ya kuangamiza nyuki hao.

"Hili tukio lilipotokea tuliwasiliana na mamlaka zinazohusika na tayari wamefika kwa ajili ya kuwaangamiza nyuki hawa ambao wamekuwa ni tishio na kuondoka na uhai wa huyu mwenzetu,"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top