Watu wawili wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kata ya Nkininziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora saa 12 asubuhi Novemba 5, 2021.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao magari mawili yaligongana uso kwa uso huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa lori aliyehama upande na kuigonga Noah.
Katika ajali hiyo waliofariki ni mchungaji Nathanael Magomola (60) na Recho Msengi (60) wote wakazi wa Tabora.
Watu watatu wamejeruhiwa katika ajali hiyo na wanaendelea na matibabu hospitali ya Rufaa ya mkoa Kitete.