AMUUA EX -WAKE KWA KUKATAA KURUDIANA NAE

0

 


Polisi nchini Kenya wanachunguza tukio la Mwanafunzi wa Kidato cha Nne, Douglas Kipchumba (21) kumbaka na kisha kumuua Mpenzi wake wa zamani na baadaye kumtupa Mtoto wa EX wake Mtoni  na yeye kuamua kunywa sumu.

Tukio hilo limetokea  eneo la Sosiani mjini Eldoret ambapo Kipchumba anadaiwa kumbaka na kumuua EX wake ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu, Hilda Kosgey aliyekuwa anaishi nae pamoja kabla ya kuachana, hata hivyo sumu aliyokunywa aikumuua na sasa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Mashuhuda wanasema chanzo cha mauaji hayo ni Mvulana huyo kumlazimisha EX wake warudiane lakini akawa anakataa, inadaiwa pia kuwa Mtoto ni chanzo cha ugomvi kwakuwa Mvulana huyo alikuwa anadai Mtoto ni wake huku Msichana akisema sio wake.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top