Daktari wa mifugo wa kijiji cha Loiborsoit A wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Malipe Ole Kisota ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu waliomtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao.
Imeelezwa kuwa alikatwa na sime sehemu mbalimbali mwilini na ndugu watatu, Lazaro, Mamei na Supek Mamei, wakimtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao Kinaruu Mamei.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza Novemba 13,2021 ameieleza Mwananchi Digital kuwa mauaji hayo yametokea Novemba 11,2021.
"Mwanamke alipohojiwa alikubali kuwa na mimba ya mtu mwingine ndipo mume wake akachukua uamuzi wa kikatili wa kumuua akishirikiana na ndugu zake," amesema kamanda Mwakyoma.