Soko la Manzese katika mji wa Tunduma mkoani Songwe limeteketea kwa moto kuanzia majira ya saa 12 asubuhi na hadi kufikia saa mbili asubuhi ya leo (Nov.16.2021)
Jeshi la zimamoto na uokozi mkoani humo lilikuwa bado linaendelea na uzimaji moto huo ili kutosababisha madhara zaidi.
Mpaka sasa haijabainika chanzo cha moto huo ni nini,huku jeshi La zimamoto likisema litatoa taarifa baadae.
Taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu! Zitakujia hivi punde!
Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, unateketeza maduka yaliopo katika soko la Manzese - Tunduma mkoani Songwe |