🔴DADA POA WADAIWA KUKWAMISHA VIJANA KUOA KISARAWE!

0


JESHI la Polisi wilaya ya Kisarawe limesema vijana wanashindwa kuoa mapema kwa sababu huduma ambayo walipaswa kupatiwa na wake zao baada ya kuoa wamekuwa wakiipata kwa bei nafuu kutoka kwa wadada poa wanaofanya biasahra ya ngono wilayani humo.


Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wilaya ya Kisarawe, Eva Steshen wakati wa ziara iliyofanywa na kamati ya UKIMWI iliyobaini kuwepo kwa madanguro wilayani humo.

Aidha, madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo wamesema kufuatia kuibuka kwa vikundi vya wasichana wanaojihusisha na uuzaji wa miili yao wilayani humo, wameanzisha mpango wa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na mikopo kama mitaji itakayowawezesha kuachana na vitendo hivyo badala ya kuwafukuza.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata wa Kibuta wilayani Kisarawe mkoani Pwani Mhandisi Mohamed Kilumbi, amesema kuwa Kata ya Mbuyuni wilayani humo inakabiriwa na upungufu mkubwa wa Condom na kuiomba kamati ya kupambana na UKIMWI kuchukulia kwa uzito jambo hilo na kuharakisha kuzipeleka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top