Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba, Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Shein Mohamed Shein kilichotokea jana (Novemba 14,2021).
Katika salamu hizo za pole, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kusikitishwa kwake na kifo hicho na kumtakia pole na ustahamilivu Rais Mstaafu Dk. Shein na Familia yake katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
SOMA HII; Kijana auawa kwa kuchepuka na mpenzi Wa jirani yake
Rais Dk. Mwinyi na Familia yake wamemuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Marehemu Mzee Shein Mohamed Shein amlaze mahala pema peponi, Amin.