FAMILIA YAPIGA KAMBI ZIWANI KUSUBILI MAITI YA MTOTO WAO ALIYEULIWA NA MAMBA!

0

 


Familia moja katika kijiji cha Katuit cha Loruk kaunti ndogo ya Baringo kaskazini iko katika majonzi huku juhudi zao za kuopoa mwili wa msichana wao mdogo aliyeshambuliwa na mamba katika Ziwa Baringo miezi mitatu iliyopita zikiendelea kutozaa matunda. 

Cherop Sangut, mwenye umri wa miaka 13, alishambuliwa kwenye ufuo wa Ziwa Baringo ambako alikuwa ameenda kufua nguo na kuoga - alasiri ya Agosti 9 - 2021.

 Kulingana na mashahidi, mamba mkubwa alimrukia na kumshika kwenye taya zake kabla ya kumtumbukiza kwenye kina kirefu cha maji. 

Marafiki zake waliokuwa naye walijaribu kumtoa mikononi kwa kumshika miguu, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda 

Mamake Sangut, Toyoi Lokodong mwenye umri wa miaka 35, amekuwa akizunguka ufukweni, akitumai kupata mwili wa msichana wake aliyekufa, au chochote kilichosalia chake ili familia iweze kumzika kwa heshima. 

Leo familia ambayo tayari inateseka chini ya hali mbaya ya umaskini, inaomba msaada kwa serikali na wadau.

Familia hiyo imepiga kambi katika ufuo Wa ziwa wakiwa wamejenga kibanda chao kidogo kwa vijiti na karatasi za plastiki wakiendelea kuweka tumaini la kuupata mwili wa mtoto wao.

 Familia hiyo maskini imemtaja Cherop kuwa msichana mwenye nidhamu, mcheshi na mchapakazi.

 "Moyo wangu bado haujakubali kwamba binti yangu mrembo mzaliwa wa kwanza amekufa na ameenda," mama alisema

 Tangu kutokea kwa mkasa huo, amekuwa akizunguka mwambao wa ziwa iwapo upepo mkali unaweza kusukuma sehemu ya mwili inayotambulika ufukweni 


Naibu Mlinzi wa Huduma ya Wanyamapori ya Baringo David Cheruiyot alisema hii ni mara ya kwanza wanalazimika kushughulikia kesi ambapo mwili wa mwathiriwa hupotea kabisa baada ya shambulio kama hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top