JE! SHERIA INARUHUSU KUCHUKUA MALI YA UNAYEMDAI KWA NIA NJEMA YA KUDAI HAKI BILA NIA YA KUIBA

0

KIFUNGU CHA 9 CHA KANUNI YA ADHABU SURA YA 16.
𝐁𝐨𝐧𝐚𝐟𝐢𝐝𝐞 𝐜𝐥𝐚𝐢𝐦 𝐨𝐟 𝐫𝐢𝐠𝐡𝐭 (kudai haki kwa nia njema), ni moja ya kanuni kuhusu uwajibikaji wa kijinai ambayo inampa kinga mtu aliyenyang'anya mali ya mtu mwingine kwa nia njema ya kuhakikisha anapata haki yake kutoka kwa mtu huyo.

𝐌𝐟𝐚𝐧𝐨. "A", anamdai "B" kiasi cha fedha jumla ya Tsh. 50,000 hivyo akaamua kuchukua "simu" ya "B" kwa lengo la kuhakikisha analipwa fedha zake na mtu "B". Katika mazingira kama haya, "A" hatahesabiwa kuwa ametenda jinai kwakuwa amefanya kwa nia njema ya kudai haki yake.

Kinga hii ipo katika mali pekee, jinai inayofanywa kuhusiana na mali kwa nia njema ya kudai haki hulindwa na kanuni hii, kanuni hii haiwezi kupewa kinga katika JINAI zingine. Hairuhusiwi kumpiga, kumuumiza, au kufanya kitendo chochote ambacho ni kiso kisheria kwa lengo la kudai fedha au haki fulani kutoka kwa unayemdai.


Imeandikwa na Mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)

Wa Jungu la sheria Tanzania

0758218269/0628729934

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top