đź”´KIJANA WA MIAKA (19) AUAWA KATIKA FUMANIZI NA MPENZI WA JIRANI YAKE!

0

 

Picha haihusiano na tukio la habari hii

Kijana mmoja aitwaye Lavunje Chubwa (19) ameuawa Mkoani Geita baada ya kufumaniwa akiwa na Naima Abdul (26) ambaye ni Mpenzi wa John Helman na walikuwa wanaishi wote nyumba moja. 


John Helman (27) licha ya kwamba hajamuoa Naima lakini walikuwa wanaishi nyumba moja na Lavunje Chubwa aliingia kwenye nyumba ya John akawa anastarehe na Naima kabla ya John kuwafumania wakiwa wamejifungia na alipowataka kufungua mlango waligoma.


RPC wa Geita Henry Mawaibambe amesema baada ya kutokea tukio hilo John aliupa taarifa Uongozi wa Kijiji na wakauvunja mlango na kusababisha Lavunje Chubwa kuruka ukuta na kuangukia chumba kingine kisha kuvunja mlango na kukimbia ambapo wananchi walimfukuza na kumkamata na kisha kwa hasira John Kafuku alimjeruhi Lavunje kichwani kwa kutumia fimbo.


"Lavunje alikimbizwa katika Hospitali ya Bwanga na Badae hospitali ya Rufaa Geita na amefariki wakati akipatiwa matibabu, chanzo cha tuki ni wivu wa kimapenzi na ukosefu wa maadili, John na Mpenzi wake Naima wote wamekamatwa kwa mahojiano" — RPC Geita

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top