SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20 ILIYOREJEWA MWAKA 2019.
KIFUNGU CHA 147.Mtu yeyote aliyeitwa kuhudhuria kama shahidi ambaye, bila sababu ya msingi, anashindwa kuhudhuria kama alivyotakiwa na wito au ambaye, baada ya kuhudhuria, anaondoka bila kupata ruhusa ya mahakama au anashindwa kuhudhuria baada ya kuahirishwa kwa mahakama baada ya kuamuriwa kuhudhuria, atawajibika kwa amri ya mahakama kulipa faini isiyozidi shilingi elfu tano.
Faini iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha kwanza inaweza kutozwa kwa kushika na kuuza mali yoyote inayohamishika inayomilikiwa na shahidi ambayo iko ndani ya mipaka ya eneo la
mamlaka ya mahakama.
Ikishindana kupata faini kwa kushika mali na kuuza shahidi anaweza, kwa amri ya mahakama, kufungwa kama mfungwa wa madai kwa kipindi cha siku kumi na tano isipokuwa kama faini imelipwa kabla ya kuisha kwa kipindi hicho.
Kwa sababu nzuri itakayoonyeshwa, Mahakama Kuu inaweza kusamehe au kupunguza faini yoyote iliyotolewa chini ya kifungu hiki na mahakama ya chini.
Imeandikwa na,
Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa @yesayajm_
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934.