Imeelezwa kwamba hadi kufikia Desemba 2021, Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe itakuwa imemaliza kulipa madai yote ya asilimia 5 za wakusanyaji mapato wa vijiji ambazo inadaiwa
Picha kutoka kikao cha baraza la Madiwani makete waliohoji asilimia 5% ya makusanyo ya mapato vijijini wiki jana |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bw. William Makufwe amekiri kuwepo kwa madai hayo na kusema tayari wanaendelea kuyalipa na mpaka kufikia Desemba mwaka huu wanatarajia kukamilisha madeni hayo yote
Amesema kutolipa kwa wakati kunasababisha watendaji wanaokusanya mapato kuingiwa na tamaa ya kutumia fedha za serikali wanazokusanya na kujikuta wakijiingiza kwenye matatizo
Baadhi ya madiwani hao wametaka kufahamu ni hatua gani ambazo zinachukuliwa kwa watendaji ambao wamehama na kuacha madeni kwenye POS zao huku wengine wakihamishwa ilihali wameondoka na fedha za michango ya wananchi
Kuhusu watendaji waliotumia fedha za serikali kinyume cha utaratibu Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Hawa Kada akijibu kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo ya mipango na fedha Mh. Francis Chaula amesema hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa dhidi ya watendaji wa aina hiyo
Mkurugenzi Makufwe amesema watendaji wote walioondoka na fedha za michango ya wananchi, wataorodheshwa ili hatua zichukuliwe na fedha hizo watazilipa
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Apollo Laizer amesema kwa watendaji ambao walikula fedha za serikali na wakapoteza sifa za kuwa watumishi wa umma, serikali ya kijiji ninatakiwa kufungua kesi ili fedha hizo zilipwe.
Credit;-Edwin Moshi-Greenfm