Mwanamke Esther Mummy anashtakiwa kwa kuteketeza moto nyumba ya mumewe waliyetengana na kusababisha hasara ya Sh4.8milioni.
Esther Mummy Webisa mwenye umri wa miaka 37 alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Bw Derrick Kutto kwa kuteketeza nyumba ya mumewe katika mtaa wa Akiba eneo la South C Nairobi.
Mbali na nyumba ya mumewe Fulgence Gaspe Assenga pia moto ulisambaa na kuchoma nyumba ya jirani yake Stella Mkafitina.
SOMA HII; Kijana auawa kwa kuchepuka na mpenzi Wa jirani yake
Esther alikabiliwa na shtaka la kuchoma nyumba mbili za makazi.
Katika shitaka hill Mtuhumiwa Alikana kuchoma nyumba ya Fulgence na Mkafitina zenya thamani ya Sh4,821,200.
Esther adaiwa alisafiri kutoka Bungoma Oktoba 28 kumtembelea mumewe waliyetengana.
Alipowasili Mshtakiwa alipiga simu mumewe haikujibiwa kisha akakwea ukuta akaingie mle ndani na kudaiwa alimwumiza mumewe mkono.
Mumewe alienda kutoa ripoti katika kituo cha polisi na akiwa polisi alipokea ujumbe nyumba inaungua moto.
Maafisa wa polisi na maafisa wa idara ya wazima moto ya kaunti ya Nairobi waliuzima moto huo na Esther alikamatwa eneo LA tukio.
Mlalamikaji wa pili alilieza mahakama kunusirika ateketee ndani ila aliokolewa na majirani.
Mtuhumiwa Esther aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1milioni moja ambapo kesi yake itakapotajwa tena Novemba 18 mwaka huu.