DC JUMA SWEDA |
Na Edwin Moshi-MAKETE
Mamlaka ya Maji Makete Mjini imeagizwa kuacha kuwabambikia ankara (Bill) za maji kwa wateja wao kwa kuwa suala hilo ni kinyume na maagizo ya Wizara ya maji
Akiwa kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa kata ya Iwawa wilayani hapo Novemba 11, 2021 wananchi hao wameeleza changamoto mbalimbali za maji ikiwemo mgawo wa maji, pamoja na mita kusoma kiwango kikubwa kuliko matumizi hayo
"Maji mtaa wa Dombwela ni tatizo kwa wiki tunapata maji mara moja ikizidi sana mara mbili na penyewe kwa masaa na yakija unakuta kila mtu amekinga ndoo moja maji yamekatika" Nofath Kyando mkaazi wa iwawa.
Hali hiyo ikamfanya Mkuu wa wilaya kumuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Makete Mjini Mhandisi Yonas Ndomba kujibu maswali hayo ya wananchi ambapo amesema ni kweli kumekuwa na changamoto ya mgawo wa maji ambao umesababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi hali iliyopelekea maji kupungua katika vyanzo wanavyovitumia
'kwa kipindi hiki kuanzia mwezi wa kumi na huu wa kumi na moja vyanzo vyetu vyaa maji vipepungua maji kutokana na ukame ndio kuna tatizo hilo,lakini mvua ingekuwa imeanza kunyesha tungekuwa na maji mengi zaidi'
Mhandisi huyo pia amekiri kuwepo na changamoto ya viluilui katika maji yanayokwenda kwenye kitongoji cha Mpangala kutokana na maji yake kutokuwa na tenki hivyo ili kuondokana na changamoto hiyo wataweka dawa kwenye chanzo cha maji ili kuua vijidudu
Ndipo Mkuu huyo wa wilaya akalazimika kumuagiza mhandisi huyo kutatua Changamoto hizo ikiwemo kuacha kuwabambika ankara ambapo pia amewataka wananchi hao kutolipa ankara ambayo msoma mita hatawashirikisha na endapo wakiwakatia huduma ya maji wananchi hao wakaripoti kwake
"mimi siwezi uridhika hivyo nyie si wataalam mnajua ikifika mwezi wa nane watisa wakumi mvua haipo sasa nataka ukarekebishe,nataka maji yatoke ambako hayatoki,ukafanye kazi mimi siko hivyo nataka utumie akili yako kutatua tatizo sio kuniambia kuna tatizo halafu umeliacha na unajua kila mwaka lipo,na ukitaka upate hela lazima watu wapate maji' amesema DC Juma.
Kuhusu kubambikiziwa wananchi bili za maji mkuu wa wilaya amesema 'Ili uelewane na mimi sitaki dhuruma kwa watu kama bili imesoma mbili chukua ya kwako nenda usijiongezee mapato ambayo si ya kwako nataka tuelewane watu wa Makete kama kuna bili zinasoma afu wanasoma wenyewe hawakushirikishi hiyo bili usilipe.'amesema DC Juma.