MTOTO AUAWA SABABU YA DENI LA TSH.3,000/=

0

 

Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Suye jijini Arusha, Evance Florian (17) ameuawa kwa kipigo ikielezwa kuwa chanzo ni deni la Sh.3000.

Akizungumza na Mwananchi Digital Jumapili Novemba 14, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo amesema mwanafunzi huyo amefariki jana akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru na akifafanua chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo ni kupigwa.

Amesema jeshi hilo linamshikilia mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha, Ibrahim Shaban (18) kwa madai ya kumpiga kijana huyo Florian na kumsababishia kifo.

Kamanda Masejo amesema uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika jarada litafikishwa katika ofisi ya mashitaka kwa hatua za kisheria.

Amesema mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru .

Credit;Mwananchi


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top