MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AHUKUMIWA MIEZI SITA NA KULIPA FAINI YA TSH. 85,000/

0

 Hukumu ya kesi ya jinai namba 53 ya mwaka 2021 dhidi ya Anna Sanga (36) wa kijiji cha Lupalilo wilayani hapo pamoja na mwanafunzi wa shule ya msingi Lupalilo (13) ambaye ni mwanae walioshtakiwa kwa makosa ya wizi wa vitu mbalimbali vya ndanj imetolewa.
Imeelezwa katika mahakama ya Wilaya ya Makete kuwa washtakiwa hao mnamo Septemba 4, 2021 majira ya saa 5 asubuhi  mlalamikaji aitwaye Sara Sanga (50) aliibiwa vitu mbalimbali vya ndani ikiwemo meza viti na vyombo vyenye thamani ya shilingi laki nane na elfu themanini na tano.

Hata hivyo upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wake dhidi ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Anna Sanga mama mzazi baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani pasipo shaka.

Mahakama hiyo imemhukumu mwanafunzi huyo wa shule ya msingi Lupalilo (mtoto wa Anna Sanga) kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya shilingi 85,000 kwa mlalamikaji .

Utekelezaji Wa faini mahakama imemtaka Mwanafunzi Hugo kulipa ndani ya Sikh 30,tangu Siku ya hukumu hiyo kutolewa huku mama akiachiwa Hutu.

Hukumu hiyo imetolewa Novemba 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Makete Mh. Ivan Msaki pamoja na mwendesha mashtaka wa serikali Asifiwe Asajile.

Chanzo;Greenfm radio Makete

Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top