MWENYEKITI WA KITONGOJI ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA WIVU WA KIMAPENZI

0

Picha hii haina uhusiano na tukio hili!

Mwenyekiti wa kitongoji cha Urua chini,kijiji cha Mfuruashe wilayani Rombo,Agustine Moshi(35) amemuua mkewe, Anastasia Agustine (31) kwa kumkata kata na kitu chenye ncha kali na kisha mwenyewe kujiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mshereheshaji maarufu wilayani humo (MC), anadaiwa kutenda mauaji hayo usiku wa kuamkia leo Novemba 8, 2021.


Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Novemba 8, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema wawili hao walikuwa na mgogoro wa kimapenzi, ambapo wiki moja iliyopita mke wake huyo alimpeleka dawati la jinsia Rombo.
"Huyu jamaa wiki iliyopita mke wake alimpeleka dawati la jinsia hapa wilayani, walisuluhishwa lakini inaonekana halikuisha na ni suala ambalo inaonekana ni wivu wa mapenzi, hivyo akaamua kuchukua jukumu la kumuua mkewe na kisha kujiua kwa kujinyonga," amesema Kanali Maiga.
Kanali Maiga amesema wanandoa hao wameacha watoto watatu wadogo.
Credit;Mwananchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top