Mimi na mume wangu hatuna tatizo, lakini shida nikuwa, kuna Kaka nimekutana naye kwenye mahusiano, yeye kaoa ndoa yake ina mwaka mmoja tu. Ananisumbua balaa mpaka natamani kufa kaka. Iko hivi, tangu kuo huyo Kaka hajabahatika kupata mtoto, kuna kipindi aliniambia kwa anahisi kuwa mke wake ana matatizo na kuniomba mimi nimzalie.
Mwanzo nilikataa, lakini baadaye alinialewesha na kuniambia kuwa, yeye hahitaji kumchukua mtoto, anataka tu nibebe mimba yake ili kujiona kama ana matatizo au la na mimba nimpe mume wangu alee. Kwakua nilikua nampenda nilimkubalia, tukahangaika kutafuta mtoto lakini na kweli mwezi wa tano mwaka huu nilibeba mimba yake.
Baada ya kubeba ujauzito wake kweli alinionyesha mpenzi, alikua ananijali, nikipiga simu hata usiku atakuja nyumbani kwangu na kukaa nnje ya geti, hata nikikaa masaa mawili sitoki atanisubiria, nitafauta sababu ya kumtoroka mume wangu usiku ili tu kumuona. Alikua ananihudumia, wakati mwingine namuambia amtumie mke wake meseji mbaya ananisikiliza kwakua tu nina mimba yake.
Wiki mbili Kaka niliona kama mwanaume kabadilika, ujauzito wangu ni mkubwa una miezi sita sasa, nikaona mtu hajali tena, simu hapokei, yaani hata kunihudumia hanihudumii tena. Nilipochunguza nikagtundua kuwa kumbe mke wake ana ujauzito ingawa wake ni mdogo. Niliumia sana lakini nilihangaika nikamtafuta na kumuona, anachoniambia Kaka nikuwa mtoto nimpe mume wangu au kama vipi nitoe mimba.
Kaka mume wangu anajua kuwa ujauzito ni wake lakini si kweli, nampenda sana huyu kaka, natamani hata kumtafuta mke wake kumuambia ukweli kuwa nina ujauzito wa mke wake. Yaani kaka sijui hata nifanye nini, najihisi kuchanganyikiwa, kila nikiwaza jinsi alivbyokua ananipenda nashindwa cha kufanya. Mume wangu haninyanyasi lakini hana mapenzi, yuko bize na kazi hata kujibu meseji hawezi, yaani namiss sana huyo kaka na sijui nifanyen nini?