Kijana Frank Sanga (23) Mkazi wa kijiji cha Iniho wilayani Makete mkoani Njombe amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka (13) (jina limehifadhiwa) mkazi wa kijiji cha hicho cha Iniho
Soma Hii.Baba amuua mwanae kisha kumzika shimoni
Imeelezwa kuwa mnamo Oktoba 7, 2021 katika kijiji cha Iniho mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la kumbaka mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Iniho kinyume na kifungu cha 130 (1)(2e)cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2019.