SERIKALI YAPOKEA DOZI ZINGINE ZA CHANJO YA COVID 19

0

 Serikali ya Tanzania imepokea Dozi 499,590 za Chanjo ya Uviko-19 aina ya Pfizer -Biontech ikiwa ni awamu ya tatu ya upokeaji chanjo kupitia mpango wa Covax Facility.

Akizungumza katika hafla fupi ya upokeaji wa chanjo hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wasee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amesema ujio wa chanjo hiyo utasaidia kuokoa maisha ya zaidi wananchi laki mbili, huku takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia Novemba 19, 2021 jumla ya wananchi zaidi ya milioni moja na laki tatu wameshapatiwa chanjo za Janssen na Sinopharm.


Akizungumzia ujio wa Chanjo dozi hizo, Waziri Dk. Gwajima amesema zitasaidia watanzania kwa na fursa ya kuchagua chanjo anayotaka, ambapo hadi sasa chanjo aina tatu tofauti zimeingizwa nchini kupitia mpango huo wa COVAX Facility. Chanjo hizo ni Janssen, Sinopharm pamoja na Pfizer ambayo imewasili leo.


Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright amesema chanjo hiyo itasaidia kupunguza athari ya kusambaa kwa maambukizi ya Uviko-19 Tanzania ambapo ameihakikishia serikali ya Tanzania, kuwa Marekani watakuwa bega kwa bega


Naye Mwakilishi wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Laurence Malangwa, amesema wamejipanga kuhakikisha dozi hizo zinatumiwa na wananchi kwa haraka ili kufikia lengo la kudhibiti ugonjwa huo kwakuwa Dar es Salaam ndio lango kuu la kuingilia na kutokea wageni mbalimbali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top